Malawi kudhibiti biashara ya fedha za kigeni baada ya sarafu yake kuporomoka

0
18

Malawi imetangaza hatua mpya za kudhibiti biashara ya fedha za kigeni na kupambana na wafanyabiashara wa magendo baada ya thamani ya sarafu yake, Kwacha, kushuka.

Sarafu ya Kwacha ilishuka thamani kwa asilimia 30 dhidi ya dola ya Marekani, na sasa mauzo ya fedha za kigeni kwenye benki na taasisi nyingine za kifedha hayataruhusiwa kuvuka dola 2,000.

Waziri wa Fedha, Simplex Banda amesema hatua hizo zinalenga kurejesha utulivu kwenye soko la fedha huku akielekeza msako dhidi ya wafanyabiashara haramu wa fedha.

Serikali pia imefanya mashauriano na Benki ya Dunia na mashirika mengine ya kimataifa kuhusu kuongeza misaada kwa watu masikini kupitia programu ya serikali, hatua inayolenga kuwalinda watu masikini dhidi ya athari za kuporomoka kwa thamani ya sarafu.

Hii ni mara ya pili kwa Malawi kushusha thamani ya sarafu yake, na hatua hii imezua malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi, ambao wanapanga maandamano.

Send this to a friend