Malawi: Wawili wakamatwa kwa kuiba zulia la Rais na hema

0
44

Polisi nchini Malawi wanawashikilia wanaume wawili kwa tuhuma za kuiba zulia jekundu la Rais Dkt. Lazarus Chakwera kutoka kwenye gari la Wizara ya Uchukuzi na Utumishi wa Umma.

Taarifa iliyotolewa na polisi imeeleza zulia hilo limepatikana baada ya uchunguzi kufanyika, na watuhumiwa hao waliotajwa kuwa ni Lino Richard na Jonasi Harold, wote wenye umri wa miaka 20 wanahojiwa.

Zulia hilo liliibwa pamoja na hema usiku wa kuamkia Jumatano wakati samani hizo zikihamishwa kuelekea wilayani Mwanza nchini humo ambapo Rais Chakwera anatarajiwa kufanya ziara.

Tukio hilo linakuja siku chache baada ya watu wasiojulikana kuvamia ofisi ya Makamu wa Rais, Saulos Chilima katika mji mkuu wa Lilongwe na kuiba baadhi ya vitu.

Send this to a friend