Malawi yakabiliwa na uhaba wa mafuta, nauli zapanda

0
41

Malawi inakabiliwa na uhaba wa mafuta unaopelekea misururu mirefu ya magari katika vituo vya mafuta yanayosubiri kwa saa kadhaa na wakati mwingine usiku kucha kwa matumaini ya kupata mafuta.

Mdhibiti wa nishati nchini Malawi amesema nchi hiyo imemaliza akiba yake ya mafuta hasa kutokana na ukosefu wa fedha za kigeni.

Uhaba wa mafuta umewalazimu waendeshaji wa magari ya umma kupandisha gharama karibu mara mbili ya nauli zao, lakini bado wanadai licha ya kupanda kwa nauli, hawapati faida yoyote kwa sababu wanatumia siku moja au mbili kupanga foleni ya mafuta bila kufanya biashara yoyote.

“Watu wengi hapa wanategemea mabasi madogo. Kwa hiyo tatizo hili limetuathiri sana kwa sababu hata familia zetu zinaishi kwa sababu ya biashara hii na uhaba wa mafuta ni pigo kubwa kwetu,” amesema Calisto Kambani, mmiliki wa biashara ya mabasi madogo mjini Blantyre

Afrika Kusini kubinafsisha shughuli za bandari kwa kampuni ya Ufilipino

Malawi imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa mafuta wa mara kwa mara tangu mwezi Agosti mwaka jana kwa kiasi kikubwa kutokana na kwamba nchi hiyo haina fedha za kigeni za kutosha.

Benki Kuu ya Malawi ilisema mwezi Juni kwamba akiba ya serikali ya fedha za kigeni haitoshi kudumu hata kwa mwezi mmoja.

Serikali ya Malawi imewatoa hofu wananchi wake na kuelezea kwamba uhaba wa mafuta uliopo ni wa muda na utamalizika ndani ya siku tatu.

Send this to a friend