Malawi yaondoa zuio la mahindi kutoka Tanzania

0
50

Serikali ya Malawi imeondoa zuio la mahindi ya Tanzania kuingia nchini humo, zuio ambalo liliwekwa kwa kile walichosema kuwa ni kutokana na kuwepo kwa ugonjwa wa mahindi wa ‘Necrosis’ (MLND) nchini.

Katika taarifa ya Wizara ya Kilimo ya nchini Malawi imesema imekuwa ikiwasiliana mara kwa mara na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu nchini ili kupeana taarifa kuhusu maambukizi ya ugonjwa huo ambapo Tanzania imethibitisha kuwa ugonjwa huo umedhibitiwa.

Bashe: Upungufu wa sukari nchini utaisha Machi, 2024

“Kutokana na hali hii, wafanyabiashara wanaruhusiwa kuagiza mahindi kutoka Tanzania baada ya kupata idhini na nyaraka zinazohitajika, ikiwa ni pamoja na idhini za afya na mimea kutoka mamlaka ya Malawi na Tanzania,” imeeleza.

Naye, Waziri wa Kilimo wa Tanzania, Hussein Bashe amesema tayari ameiagiza mamlaka ya afya ya Mimea na Viuatilifu kuondoa zuio kwenye mpaka wa Kasumulo na kuruhusu magari ya soya na mahindi ya Malawi kupita, na ikiwa mabadiliko yoyote yatatokea hatua stahiki zitachukuliwa.

Send this to a friend