Malawi yapiga marufuku uagizaji mahindi toka Kenya na Tanzania

0
51

Malawi imezuia uagizaji wa mahindi kutoka Kenya na Tanzania kwa sababu ya wasiwasi wa kuenea kwa ugonjwa hatari wa Mahindi, Lethal Necrosis ambao unaweza kuharibu akiba ya chakula nchini humo.

Uamuzi huo umetokana na hofu ya uhaba wa chakula ambao unaathiri zaidi ya watu milioni 4 nchini humo ambapo kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo ya Malawi, ugonjwa huo hautibiki na unaweza kusababisha upotevu wa mavuno kwa kiwango cha asilimia 100.

Mtaalamu wa kilimo, Henry Kamkwamba, ameeleza kuwa marufuku hiyo itasaidia kulinda Malawi dhidi ya ugonjwa huo, akiongeza kuwa uingizaji wa mahindi usiosindikwa unaweza kuwa hatari kwani baadhi ya mahindi hayo yanaweza kutumika kama mbegu.

“Kama mnavyofahamu baadhi ya mbegu tayari zimeharibika kutokana na ukame wa muda mrefu na watu wanapanda kwa mara ya pili. Tukiagiza baadhi ya mahindi haya, kuna uwezekano kwamba baadhi ya mahindi ambayo yataingizwa nchini, yanaweza kutumika kama mbegu ingawa hayajapendekezwa kama mbegu,” amesema.

Ruto: Kupanda kwa gharama za maisha sio tatizo la Serikali

Ameongeza kuwa “fikiria jinsi tulivyopoteza ndizi zetu zote siku za nyuma na sasa Malawi ni mwagizaji wa ndizi kwa sababu ya masuala fulani yanayotokana na sera zetu zisizo makini katika suala la uagizaji. Tuliishia kuagiza virusi vilivyojaa kwenye ndizi. Na kuna wasiwasi kama huu kutokea kwenye mahindi.”

Kenya na Tanzania mara nyingi zimekuwa vyanzo muhimu vya mahindi kwa Malawi wakati wa matatizo ya ukosefu wa chakula.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mahindi yanaweza kuingizwa nchini humo mara tu yanaposindikwa, ama kama unga au mbegu.

Send this to a friend