Mama amchoma mwanae mikono kisa TZS 30,000

0
48

Katika hali ya kushangaza mwanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Shahende, Kata ya Butobela wilaya ya Geita mkoani Geita , Helena Mashaka (13) amechomwa mikono  kwa moto na mama yake hali iliyosababisha kushindwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi.

Mtendaji wa Kijiji, Edar Michael amesema tukio hilo lilitokea saa 2 asubuhi Oktoba 5, 2022, na kwamba alipokea taarifa la tukio hilo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo.

Aliyeambiwa ana saratani na kutolewa tezi kimakosa azidai hospitali milioni 500

Amesema baada ya kupokea taarifa za tukio hilo walichukua  hatua za kumfuatilia mzazi huyo na kisha kumkamata ambapo  baada ya kuhojiwa mama huyo alidai kuwa binti yake alimwibia fedha TZS 30,000, na kuchukua maamuzi ya kumchoma moto mikono.

Edar amesema walifanikiwa kumkamata na mpaka sasa yupo kituo kidogo cha polisi Bukoli na mwanafunzi amepelekwa Zahanati ya Bukoli kwa ajili ya kupatiwa  matibabu.

Send this to a friend