Mama amuua kwa moto mtoto wake baada ya kuiba TZS 2,800

0
114

Polisi Kaunti ya Kisumu nchini Kenya wanamshikilia mwanamke anayejulikana kwa jina la Jacinter Akinyi (47), kwa tuhuma za kumchoma moto na kumsababishia kifo mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 12 baada ya kudaiwa kuiba shilingi za Kenya 150 [TZS 2,800].

Mwanamke huyo anadaiwa kumwagia mafuta ya taa mtoto wake kwenye sehemu zake za mwili na kisha akawasha moto, kitendo kilichomsababishia majeraha ya moto kwa zaidi ya asilimia 90.

Hata hivyo, majirani walimwokoa mtoto huyo na kumkimbiza hospitali, lakini alifariki kutokana na majeraha makubwa sehemu za juu za mwili, mikono na sehemu za siri.

Polisi walipofika eneo la tukio walikuta shati lililoungua likiaminika kuwa ndilo mtoto alivaa wakati wa tukio. Mama huyo sasa anashikiliwa na atafikishwa mahakamani.

Send this to a friend