Mama Janeth Magufuli: Nilimwalika Rais Samia kwa kumpigia simu tu

0
64

Mke wa Hayati John Pombe Magufuli, Janeth Magufuli ametoa shukrani zake za dhati kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa karibu na familia yake tangu kifo cha mume wake.

Ameyasema hayo katika maadhimisho ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa Hayati Dk John Pombe Magufuli yaliyofanyika leo Machi 17 wilayani Chato mkoani Geita ambayo yamehudhuriwa na mamia ya watu pamoja na viongozi mbali mbali.

“Naomba nikiri kukupigia simu lakini kwa bahati mbaya sikufanikiwa ila baadaye ulinipigia nikakupa mualiko huu ambao uliupokea kwa moyo mkunjufu na ukaahidi kuja ingawa haukuwa kimaandishi nashukuru sana licha ya kuwa na majukumu kitaifa na kimataifa, umeniheshimu sana,” amesema.

Mama Janeth Magufuli amesema kuwa kama familia wameandaa siku hii maalum kwa ajili ya misa ya kumuombea na kuenzi maisha ya Hayati John Magufuli

Mbali na hayo, amewaomba viongozi wote pamoja na wananchi kuungana naye katika kumshukuru Mungu juu ya Maisha ya Hayati Magufuli na kuwaomba Watanzania kuwa na mioyo ya upendo na kujaliana katika dhiki

Send this to a friend