Mama mbaroni kwa kutupa mapacha baada ya kujifungua

0
45

Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linamshikilia Roda Peter (30) mkazi wa Kata ya Kihonda, Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma ya kuwaua watoto wawili wachanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema mtuhumiwa ambaye ni mkulima anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 12 mwaka huu katika eneo la Kihonda kwa kuwaweka kwenye mifuko miwili ya ‘salfeti’ na kuwatupa kichakani.

“Siku za hivi karibuni kuna mama alijifungua na kutupa watoto wake wachanga ambao ni mapacha. Sasa katika upelelezi wetu kwa kushirikiana na wananchi tulifanya ufuatiliaji na kumbaini huyo mama, tumefanikiwa kumkamata anaitwa Roda Peter,“ amesema.

Aidha, kamanda amesema upelelezi wa tukio hilo unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa.

Send this to a friend