Shirika la afya duniani (WHO) linasema saratani ndio chanzo cha kifo cha mtu mmoja kati ya sita duniani, na hadi asilimia 50 ya aina zote za saratani zinaweza kuzuilika.
Lakini idadi ya visa vipya vya ugonjwa huo inatarajiwa kuongezeka kwa takriban asilimia sabini katika miongo miwili ijayo.
Haya ni mambo yanayoweza kupunguza hatari ya kupata saratani
• Usivute sigara wala kutumia tumbaku ya aina yoyote
• Hakikisha nyumbani kwako hamna moshi
• Kula chakula chenye afya
• Kunyonyesha kunapunguza hatari kwa mama kuugua saratani
• Hakikisha watoto wako wanapata chanjo dhidi ya hepatatis B na HPV
• Epuka kuchomwa sana na miale ya jua, au tumia mafuta yanayo kukinga dhidi ya miale hiyo
• Punguza uchafuzi wa hewa ndani na nje ya nyumba
• Jishughulishe kuupa mwili mazoezi
• Punguza unywaji wa pombe
• Jitahidi kufanyiwa ukaguzi wa mapema kutambua uwepo wa saratani.