Mambo 4 muhimu ya kuzingatia kabla ya kununua pete ya uchumba

0
139

Pete ya uchumba ni alama ya upendo inayowavusha wapenzi kutoka kwenye hatua ya awali ya mapenzi na kwenda kwenye hatua nyingine rasmi na muhimu kuelekea katika safari ya ndoa.

Pete ya uchumba kwa kawaida ni gharama kubwa, endapo unahitaji kumshtukiza mpenzi wako juu ya uchumba wenu, hakikisha unafanya chaguo lililo sahihi kwa kufuatilia mambo haya muhimu;

Mtindo wake wa maisha
Pete ya uchumba huvaliwa kwa kipindi kirefu, wanawake wengi hawapendelei kuvua pete zao ili kufanya shughuli zao, hivyo unapotaka kuchagua pete ya uchumba kwa ajili ya mpenzi wako ni vyema kuzingatia shughuli zake zaidi ili kutafuta pete inayolingana na mtindo wa maisha wa mchumba wako.

Kwanini watu huweka ‘airplane mode’ wakiwa ndani ya ndege?

Mfano; anafanya zaidi kazi zinazoweza kuchafua mikono yake (mpishi, mtaalamu wa mazingira, n.k)? Ikiwa ndivyo, unaweza kufikiria juu ya pete ambayo haina almasi, ambayo imeinuka (yenye mpangilio wa ‘prong’) kwani ni rahisi kusafisha.

 Muundo wa pete aina ya Prong

Aina ya mapambo anayopenda
Anapenda kuvaa nini kazini, katika mazingira ya kijamii au nyumbani? Angalia vitambaa anavyochagua, rangi na michoro anayopenda kuvaa, aina za viatu anazopendelea na mapambo anayovaa mara nyingi. Ingawa wanawake wengi huwa na tabia ya kuchagua, mchumba wako labda anaweza kuwa na aina ya mtindo unaomvutia zaidi.

Kipimo
Ikiwa unahitaji kujua saizi yake bila yeye kujua, jaribu kuazima pete ambayo mara nyingi huvaa kwenye kidole chake cha mkono wa kushoto au jaribu kupima kidole chake kwa kipande cha kamba wakati amelala. Njia nyingine inaweza kuwa kumwomba mama yake au rafiki yake kupata msaada wa kipimo chake.

Bajeti
Ni vyema kuchagua pete inayofaa kwa kuendana na bajeti yako. Siku zote gharama huwa zaidi ya vile ulivyofikiri, lakini kwa bahati nzuri kuna chaguzi za pete za uchumba kwa kila bajeti, hivyo usijiingize kwenye madeni yasiyo ya lazima.

Send this to a friend