Mambo 4 yatakayokusaidia kuwa na utendaji kazi bora

0
53

Mafanikio yako katika kazi kwa kiasi kikubwa yanategemea mtazamo wako na jinsi gani unatumia muda wako unapokuwa kazini au katika shughuli yoyote ile yenye manufaa kwenye maisha yako.

Fuatilia njia hizi zitakazokusaidia kuongeza ufanisi na kukufanya kuwa bora zaidi kazini;

Simamia vipaumbele vyako
Ili kuboresha utendaji wako kazini ni lazima uwe na uwezo wa kuweka vipaumbele, lazima utenganishe kati ya vitu ambavyo ni muhimu kwenye kazi yako na kwa ajili yako wewe mwenyewe, na vitu ambavyo havina faida kwenye kazi yako na maisha yako pale ambapo unakabiliana na majukumu mengi ya kila siku.

Kuwa na mawazo chanya
Njia nyingine inayoweza kuboresha utendaji wako unapokuwa kazini ni wewe binafsi kuendeleza tabia ya kuwa na mitazamo chanya kuhusu wewe mwenyewe pamoja na kazi yako. Kadri unavyozidi kuwa na mitazamo chanya unapokuwa katika kazi ndivyo unavyofungua milango yenye fursa nyingi zaidi kuja kwako na kuanza kuboresha maisha yako.

Namna 5 ya kuepuka kupatwa na kiharusi

Boresha ujuzi wako
Boresha ujuzi kuhusiana na kazi unayoifanya, na hakikisha kuwa mwajiri wako anajua kuhusiana na mipango yako. Unaweza kutafuta kozi ya ziada ambazo unaweza kuchukua ili kuboresha utendaji wako unapokuwa kazini. Pia unaweza kumuuliza mwajiri wako aina ya vitabu ambavyo vitakusaidia kuwa bora.

Kuwa na utu
Fahamu kuwa asilimia 85 ya mafanikio yako kazini yatakuja kutokana na utu na uwezo wako wa kuwasiliana vizuri na wengine unapokuwa kazini au sehemu yoyote ile. Ni muhimu sana kwako kuwa na heshima pamoja na nidhamu nzuri unapokuwa kazini pamoja na wafanyakazi wenzako.

Tabia hii itakusaidia si tu kuboresha utendaji wako, bali itawafanya watu wengine wawe wanataka kukusaidia kutokana na tabia yako ya usikivu na heshima kwao.

Send this to a friend