Mambo 5 wanayofanya wanaume kila siku yanayowakera wapenzi wao

0
58

Wanaume hufanya mambo mengi ambayo yanawakera wanawake licha ya kutowaweka wazi kuwa hawapendezwi nayo.

Haya ni baadhi ya mambo unayofanya kila siku ambayo wanawake wengi hawapendezwi;

Kufuatilia mpira
Wanaume huamisha mawazo yao na akili zao pale wanapokuwa wakifuatilia mpira na wenzao. Hali hii huwafanya wanawake kujihisi kama kutengwa, kutothaminiwa, na hudhani kama si sehemu ya maisha ya wanaume wakati wenza wao ama marafiki zao wa kiume wakiwa wanatazama mpira.

Wengine hukerwa na tabia ya wanaume kuacha kutazama mpira nyumbani, na kwenda maeneo ya  umma,  kama baa, kwa madai kuwa kutazama mpira nyumbani hakuna ‘mzuka.’

Kuwatazama wanawake wengine
Haijalishi mwanaume ana furaha kiasi gani katika uhusiano wake, atakapomuona mwanamke mrembo akipita mbele yake ama popote, atamwangalia. Jambo hili kwa wanawake wengi hawalipendi.

Kukoroma
Kujizuia kukoroma ni sayansi ngumu kwa walio wengi. Ingawa ni wazi wanawake na wao wanakoroma pia, lakini ni wanaume wanaoathirika zaidi kwa kuwa wanawake hawapendezwi kuona mtu akikoroma.

Kutoa hewa chafu hadharani
Wanaume wengi kwa asili ni watu wasio na aibu kulinganisha na wanawake. Mwanamue anaweza kujamba akiwa na wenzake, lakini mwanamke hujizuia kufanya hivyo.

Mambo 7 ambayo wanaume hawapendi yanapofanywa na wanawake

Wanawake wengi hawapendi kumuona ama kumsikia mwanaume ambaye anafanya hivyo hadharani, iwe kwa bahati mbaya ama kwa makusudi.

Kutokiri makosa
Kusema nimekosea ni kitu kigumu kwa baadhi ya wanaume, hata kama wamekosea kweli. Wapo wanaodhani kwamba wakisema wamekosea ni udhaifu, wanawake hawapendezwi na wanaume wa namna hiyo.