Mambo 5 ya kuepuka unapokwenda kutambulishwa ukweni 

0
81

Kukutana na wazazi wa mpenzi wako inaweza kuwa ishara ya uhusiano mzuri, lakini pia ni tukio la kusisimua kwani ni wakati ambapo wazazi wa binti hukuangalia kwa kina endapo unamfaa binti yao.

Kosa lolote dogo ambalo utalifanya linaweza kukutafsiri kwa njia tofauti.

Haya ni mambo 5 ya kuepuka unapokwenda kutambulishwa nyumbani kwa wazazi wa mpenzi wako.

Acha majigambo

Ni vizuri kuwa na matamanio, lakini usianze kujigamba kwa kumwambia baba yake kuwa utakuwa Mkurugenzi Mtendaji anayefuata wa kampuni fulani kubwa sana, au kujitamba kwa jinsi gani ulivyo bora. Yeye ni mzee sana kuliko wewe pia ana busara zaidi, hivyo anaweza asipendezwe na wewe.

Acha dharau

Unaweza kuendesha gari bora kuliko baba yake,  chakula cha mama yako kinaweza kuwa bora kuliko mama yake, au unaweza kuishi katika nyumba kubwa zaidi yao. Hakuna sababu ya kujaribu kuwadharau ili kutaka uonekane bora.

Kufanyia mzaha utamaduni wao

Wazazi wa binti wanaweza kutaka kukuonesha jambo fulani kuhusu utamaduni wao. Wanapofanya hivyo, hata kama unaona ni ajabu, usifanye mzaha. Bila shaka ni dharau na itaonesha kuwa huna adabu na humstahili binti yao.

Usiwaache wazazi wake wazungumze zaidi

Hata ikiwa una wasiwasi na haufurahii mazungumzo, jaribu kuzungumza na wazazi wake. Una nafasi moja tu ya kuwavutia hivyo usiwafanye waulize maswali yote na wewe kuruhusu ukimya usio wa kawaida kwa sababu tu huna la kusema.

Kubishana na mpenzi wako

Ikiwa wewe na mpenzi wako mmepishana kwa jambo fulani, jaribu kutabasamu na usubiri hadi ufike nyumbani ili mzungumze. Ni mara ya kwanza unakutana nao, kwa hivyo ungetaka kuwaonesha kwamba unamfanya binti yao kuwa na furaha. Haitasaidia ikiwa nyinyi wawili mtaanza kubishana mbele yao.

Send this to a friend