Mambo 6 ya kufanya kujikinga na ugonjwa wa figo

0
16

Wataalam wa afya husisitiza jamii mara kwa mara kujikinga na magonjwa hasa yasiyoambukiza ikiwemo ugonjwa wa figo ili kuepuka madhara makubwa yatokanayo na magonjwa hayo ikiwa ni pamoja na gharama kubwa za matibabu.

Kwa kuzingatia njia hizi zifuatazo utaweza kujikinga na ugonjwa hatari wa figo;

Epuka sigara na tumbaku
Uvutaji sigara na matumizi ya mazao ya tumbaku husababisha changamoto ya kupunguza mtiririko wa damu hivyo kupunguza uwezo wa figo kufanya kazi.

Fanya mazoezi
Mtu anapaswa kudhibiti uzito wa mwili wake, kuzingatia lishe bora na kufanya mazoezi, jambo litakalosaidia kuzuia magonjwa ya moyo na kisukari ambayo pia huchangia matatizo ya figo.

Dawa za maumivu
Jamii inatakiwa kuchukua tahadhari na matumizi ya dawa za kupunguza au kutuliza maumivu zinazonunuliwa  bila maelekezo ya wataalamu katika maduka ya dawa ambazo husababisha  uharibifu wa figo zikitumiwa mara kwa mara.

Aina ya vyakula vinavyoimarisha kumbukumbu

Kunywa maji mengi
Unywaji wa maji ya kutosha (lita 3 kwa siku) husaidia kuzimua mkojo, kutoa uchafu wote wa sumu kutoka mwilini na kuzuia mawe katika figo.

Lishe
Ulaji wa matunda na mbogamboga na kupunguza vyakula vilivyosagwa hasa baada ya umri wa miaka 40, husaidia kuzuia tatizo la shinikizo la damu. Udhibiti wa ulaji holela wa vyakula vya sukari, mafuta, nyama na chumvi huchangia changamoto za shinikizo la damu na kuwepo kwa mawe ya figo.

Dawa za Kienyeji
Unashauriwa kuwa makini na matumizi ya dawa za kienyeji, kwani kutumia bila kipimo sahihi kunaweza kuatarisha afya ya figo zako.

Send this to a friend