Mambo 5 yanayochangia kuzaa mapacha bila kufanya Matibabu 

0
96

Kuna mambo kadhaa ambayo yanaweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata mapacha bila msaada wa matibabu ya uzazi.

Kwa mujibu wa tovuti za afya za Forbes  na Healthline, haya ni mambo matano yanayoweza kuchangia kupata mapacha

Urithi

Watu wanaotoka kwenye koo zilizo na historia ya uzao wa pacha wana nafasi kubwa zaidi ya kupata watoto mapacha kuliko wale wasio na historia ya uwepo wake. Jenetiki inaweza kumfanya mtu kuwa na uwezekano wa kutoa zaidi ya yai moja, na hivyo kusababisha mimba ya mapacha,

Eneo la kijiografia

Kuna sehemu ambazo mapacha ni kawaida zaidi kuliko kwingine. Kwa mfano, kiwango cha mapacha nchini Japan ni 1.3 pekee kati ya watoto 1,000 wanaozaliwa, huku barani Afrika miongoni mwa watu wa Yoruba Kusini Magharibi mwa Nigeria, kiwango cha seti 49 hadi 53 za mapacha kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa kimeripotiwa.

Asili

Wanawake ambao ni mapacha wenyewe wana nafasi 1 kati ya 60 ya kupata mapacha, huku wanaume ambao ni mapacha  wana nafasi 1 kati ya 125 ya kuzaa mapacha.

Umri

Kulingana na Jumuiya ya Amerika ya Tiba ya Uzazi, wanawake wenye umri wa kati ya miaka 35 na 40 ambao tayari wamejifungua wana nafasi kubwa zaidi ya kupata mapacha. Hiyo ni kwa sababu wana uwezekano mkubwa wa kutoa yai zaidi ya moja wakati wa ovulation kuliko wanawake wadogo.

Muundo wa Mwili

Watu ambao ni warefu au wenye uzito mkubwa wa mwili pia huwa na uwezekano mkubwa wa kupata mapacha. Hii inaweza kuwa kutokana na tofauti za homoni zinazohusiana na utungaji wa mwili. Kwa mfano, kuwa na kiwango kikubwa cha mafuta mwilini kunaweza kusababisha kuongezeka kwa viwango vya estrojeni ambayo inaweza kuongeza uwezekano wa kutoa zaidi ya yai moja wakati wa ovulation, na hivyo kuongeza uwezekano wa kupata mapacha.