Mambo 5 yanayoweza kutokea unapotumia simu wakati unaichaji

0
64

Baadhi ya watumiaji wa simu janja ‘smartphone’ wamekuwa na mazoea ya kutumia simu inapokuwa kwenye chaji, kama kuzungumza, kutumiana jumbe au hata kucheza michezo ya simu (game).

Baada ya muda simu huonesha mabadiliko ambayo pengine hushindwa kuelewa sababu za mabadiliko hayo.

Haya ni matokeo 5 ya kutumia simu inapokuwa chaji;

Simu kuchemka
Hicho ndicho kitu cha kwanza kitakachofanyika katika simu yako ikiwa utatumia wakati imewekwa kwenye chaji. Ikiwa una mazoea haya mara nyingi tafadhali acha mara moja kwa sababu inaweza kusababisha kuvuja kwa kemikali hatari kwenye betri, kusababisha mlipuko wa betri ya simu janja yako na pengine inaweza kuzuia simu yako isiwake.

Huongeza ukubwa wa betri ya simu yako
Kuchaji simu yako unapoitumia huleta tatizo lingine, ambalo ni kuongeza ukubwa wa betri ya simu yako. Madhara yanayoweza kutokea ni kupasuka, kuwaka na kadhalika.

Hupunguza muda wa kukaa na chaji
Ikiwa hapo awali simu yako ilikuwa ikihimili kukaa na chaji takribani saa 15-18 za wastani wa muda, baada ya kuwa na mazoea ya kuitumia ikiwa kwenye chaji sasa inaweza kuwa na wastani wa matumizi wa karibu saa 7-8 au hata chini ya hapo.

Ishara 9 zinazothibitisha umekutana na mpenzi wa maisha yako (soulmate)

Huharibu chaja ya simu
Kutumia simu yako unapochaji kunaweza hata kusababisha shinikizo kwenye chaja ya simu yako, hivyo kusababisha ongezeko la joto au kutofanya kazi. Unaweza kuhitaji hata kununua chaja mpya baadaye.

Inaweza kuishia kukudhuru
Tumesikia kesi nyingi zikiripotiwa kuhusu matumizi ya simu inapokuwa chaji na wengine hupoteza maisha kwa sababu ya simu kulipuka. Ikiwa tunajali kuhusu maisha yetu basi ni vyema kuchukua tahadhali.