Wengi wetu wanatatizo la kulala chini ya saa 8 kama inavyopaswa. Tatizo hili linachangiwa kwa kiasi kubwa na msongo wa mawazo pamoja na mabadiliko ya mfumo wa maisha.
Hapa kuna mambo 5 ambayo yatakusaidia kupata usingizi zaidi:
Kula saa mawili kabla ya kulala
Hii huruhusu mfumo wa usagaji chakula kumaliza kazi yake kabla hujalala, hivyo hukupa usingizi mzuri. Ni vigumu kulala vizuri ikiwa utakwenda kulala muda mfupi baada ya kula.
Aina 10 za magari yanayotumika zaidi Dar es Salaam
Soma
Soma kidogo kabla hujalala. Kulingana na watafiti, kusoma vitabu kabla ya kulala kunaweza kuboresha usingizi wako na kuwa mtu mwenye furaha asubuhi.
Mbali na hayo, kusoma kutakupunguzia mawazo na kulegeza akili yako, hivyo kukufanya ulale haraka.
Pata mwanga wa jua asubuhi
Utaratibu bora wa usiku huanza asubuhi. Mwangaza wa jua wa asubuhi huboresha mzunguko wako wa kulala/kuamka. Inakusaidia kuamka kwa urahisi, kulala haraka na kuwa na nishati thabiti.
Punguza mwanga wa rangi ya bluu jioni na usiku
Mwanga huu hupatikana hasa katika vifaa vya kielektroniki kama simu; kompyuta, televisheni n.k.
Utafiti unaonyesha kuwa mwanga huu wa bluu hupunguza uzalishaji wa homoni ya ‘melatonin’ ambayo ndiyo hutupa usingizi. Inashauriwa kuepuka kutumia mitandao ya kijamii au kutazama vitu katika vifaa tajwa hapo juu usiku ili kuboresha usingizi wako.
Boresha mazingira ya chumba unacholala
Utafiti unaonesha kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu wanaopata matatizo ya kulala yanasababishwa na mazingira mabaya ya vyumba vyao vya kulala.
Hakikisha unalala kwenye chumba ambacho hakina mwanga mwingi, joto kali, baridi, uhaba wa hewa au kelele.