Mambo 5 yatakayokusaidia kupunguza ajali unapokuwa barabarani

0
51

Ajali za barabarani zinaweza kuzuilika endapo kila dereva atafuata sheria na taratibu za udereva. Kujiamini kupitiliza na uzembe wa baadhi ya madereva umetajwa pia kama chanzo cha ajali za barabarani.

Haya ni mambo muhimu yatakayokusaidia kuwa dereva mzuri na kuepusha ajali barabarani

Zingatia mbele
Hii ni kwa ajili ya madereva wanaopenda kuendesha gari wakiwa wanatumia simu au wakiwa kwenye maongezi na abiria. Mambo hayo yanaweza kumtoa dereva kwenye utulivu, hivyo inapotokea mtumiaji mwingine wa barabara kukatiza ghafla mbele yake huweza kusababisha ajali.

Usisogelee gari la mbele yako
Imekuwa jambo la kawaida kwa madereva kuwasogelea wenzao bila kuhofia iwapo dereva wa mbele yake anaweza kupata dharula na kufunga breki ghafla ambayo inaweza kusababisha ajali.

Epuka breki za ghafla
Iwapo utashika breki kwa ghafla huku gari la nyuma yako likiwa karibu kuna uwezekano wa kutokea ajali. Matumizi ya breki za ghafla iwe ni chaguo la mwisho, lakini muhimu ni kuhakikisha unakadiria barabara yako na hivyo unashauriwa kushika breki taratibu.

Usikae upande
Baadhi ya madereva hukaa upande jambo linalowafanya kujisahau na kukanyaga mafuta badala ya breki au breki badala ya mafuta au muda mwingine kujikuta akikanyaga vyote kwa pamoja hali inayoweza kusababisha ajali.
Mkao wa upande utamfanya dereva ahisi maumivu ya mgongo au kiuno kwenye safari ndefu, hivyo dereva anashauriwa kukaa kwa kunyooka akiwa kwenye usukani.

Kuwa mvumilivu
Dereva anashauriwa kuwa mvumilivu mara madereva wengine wanapofanya uzembe barabarani kwani anaporuhusu hasira imtawale anaweza kufanya mambo yanayoweza kusababisha ajali.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend