Mambo 6 hatari unayofanya kila siku

0
38

Kila siku tunafanya mambo ambayo yanaweza kuonekana kuwa ni salama, lakini kitaalam mambo hayo yanaweza kuwa na madhara makubwa kwa afya zetu.

Hapa kuna mambo 6 ambayo hufanywa kila siku yanayoweza kuathiri afya yako;

Maji yasiyochujwa
Ukweli ni kwamba, kunywa maji ya bomba yenye dawa au maji ya mvua bado haitupi uhalali wa kunywa maji hayo pasipo kuchujwa. Unapochuja unasaidia kuondoa bakteria ambao wanaweza kusababisha magonjwa. Watu wanaokunywa maji ya visima wanahitaji kuzingatia zaidi dawa na kuyachuja.

Dawa za maumivu
Haimaanishi kwamba haupaswi kusaidia mwili wako unapohisi maumivu, lakini ni muhimu kuwa mwangalifu na kile unachotumia na mara ngapi unatumia haswa ikiwa unatumia pamoja dawa nyingine. Unapotumia dawa hizi mara kwa mara zinaweza kusababisha uharibifu wa ini na matatizo mengine.

Kukaa kwa muda mrefu
Tafiti zinaonesha kukaa kupita kiasi kunaweza kusababisha matatizo ya kiafya kama vile; kuongezeka kwa shinikizo la damu, sukari ya damu, mafuta, maumivu ya mgongo na shingo, maumivu ya kichwa ya muda mrefu na kuongezeka kwa hatari ya kifo kutokana na ugonjwa wa moyo na saratani.

Dawa za vitamini na virutubisho
Njia bora ya mwili wako kupata lishe ni kutoka kwenye vyakula. Vidonge haviwezi kukupa vya kutosha usawa sahihi wa vitamini na madini kama inavyopaswa. Wataalam wanasema baadhi ya virutubisho vinaweza kukupa hali ya kutokwa na damu kwa wingi, pia vitamini A nyingi vinaweza kusababisha maumivu ya kichwa na uharibifu wa ini, na chuma nyingi inaweza kukufanya uwe na kichefuchefu.

Utafiti: Mtindo wa kujamiiana unaoweza kuvunja uume

Kulala kupita kiasi
Kulala kupita kiasi yaani kulala zaidi ya saa 9 kumehusishwa na hatari ya kuongezeka kwa fetma, kisukari, ugonjwa wa moyo, na kifo cha mapema. Inaweza pia kukufanya uwe na usingizi zaidi wakati wa mchana.

Kutuma ujumbe mara kwa mara
Kutuma SMS mara kwa mara kumegunduliwa kuwa na athari mbaya zifuatazo kwa afya kama maumivu sugu ya mgongo na shingo ambayo inaweza kukupa maumivu ya kichwa sugu au hata ugonjwa wa moyo, utendaji duni kazini au shuleni, usumbufu wa kwenye mahusiano, kupunguza uwezo wa kufikiria na kukupa matatizo ya macho.

Send this to a friend