Mambo 6 muhimu ya kuepuka wakati wa usaili wa kazi

0
70

Usaili wa kazi ni mchakato muhimu katika kupata ajira ambapo mwajiri anachunguza uwezo, ustadi, na sifa za mwombaji ili kufanya maamuzi ya kumpa mtu ajira au la.

Mchakato huu unaweza kujumuisha hatua kadhaa kama vile kutuma maombi, mahojiano ya awali, na mahojiano ya ana kwa ana.

Wakati wa usaili wa kazi, kuna mambo kadhaa ambayo ni muhimu kuepuka ili kuhakikisha unajiweka kwenye nafasi nzuri ya kupata fursa ya kupata kazi unayoitafuta, na haya ni mambo kadhaa ya kuepuka;

Kutochelewa: Kufika kwa wakati ni muhimu sana, hii inaonyesha nidhamu yako katika kuzingatia muda na namna ulivyo na dhamira juu ya kazi hiyo.

Kuonyesha ukosefu wa maandalizi: Ni muhimu kuwa na ufahamu mzuri juu ya kampuni unayoomba nafasi ya kazi na uwezo wako unaohusiana na nafasi unayoomba.

Kutokuwa na mawasiliano mazuri: Hakikisha unajibu maswali kwa uwazi na kwa kujiamini. Epuka kutumia lugha isiyo rasmi au yenye lugha chafu.

Kueleza mambo yako binafsi sana: Epuka kutoa habari zako binafsi sana au za kibinafsi ambazo hazihusiani moja kwa moja na kazi au uwezo wako wa kufanya kazi.

Kuonyesha ukosefu wa heshima au kujiamini kupita kiasi: Epuka kubishana na wasaili, kutoa maoni yenye kuonesha kiburi, au kuonyesha kutoheshimu wanaokufanyia usaili.

Kutotambua au kudharau swali: Ni muhimu kusikiliza kwa makini maswali ya wasaili na kujibu kwa heshima na kwa ufanisi hata kama swali lililoulizwa unaona halina mantiki.