Mambo 6 ya kuepuka unapoingia kwenye mahusiano mapya

0
64

Mahusiano mapya yanasisimua zaidi kwa wenza waliokutana. Hizi ni nyakati za furaha kwao. Lakini wataalam wa mahusiano wanasema, kipindi hiki wenza wanapaswa kuwa makini zaidi ili kuepuka makosa yanayoweza kuleta shida baadaye.

 

Haya ni mambo 6 ya kuepuka unapoingia kwenye uhusiano mapya;

 

1. Kueleza siri zako zote

Ni vizuri unapoingia kwenye mahusiano mapya kufahamiana vizuri na mwenza wako, lakini haishauriwi kuweka wazi siri zako zote. Ikiwa mengi ya mazungumzo yako yanahusu matatizo ya familia yako, madeni au magonjwa, unaweza kumtisha mwenza wako mpya.

 

2. Kupatikana sana

Wakati uhusiano wako ni mpya na mambo yanaendelea vizuri, ni kawaida kutaka kutumia wakati mwingi pamoja. Lakini haishauriwi kuonana kila wakati na hata kila mara anakapokuhitaji. Hii inaweza kushusha thamani yako mapema.

 

3. Kupuuza ishara zozote za hatari

 

Kupuuza ishara zozote za hatari za kimaadili ambazo unaziona kwa mwenza wako mpya inaweza kuwa hatari hapo baadaye. Unapokuwa katika hatua ya kwanza ya kufahamiana na mtu, ni vyema kuchukulia kwa uzito ishara zozote unazoziona kwa mwenza wako badala ya kuzipuuzia.

 

 

4. Machapisho ya mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii

Mitandao ya kijamii ni sehemu ya maisha yetu siku hizi, lakini jaribu kuepuka kutuma picha zake kwenye mitandao ya kijamii. Weka uhusiano wako kwenye mitandao ya kijamii pale utakapokuwa na uhakika nayo, na hata itakusaidia kuepuka fedheha pale yatakaposhindwa kufika popote.

 

5. Usizidishe au kuharakisha.

 

Mahusiano mapya yanaathiriwa sana na jambo hili. Mmekutana, mmependana, na kabla ya kujuana vizuri unataka kufanya kila kitu naye, kufanya ngono mchana na usiku. Kuwa mwaminifu kwako mwenyewe juu ya maadili yako ya msingi na yale ambayo ni muhimu kwako maishani.

6. Mahusiano yako ya zamani yasikuumize

 

Ikiwa ulikuwa na mwenzi wako wa zamani ambaye alikulaghai, akakufukuza, au kukuumiza kwa njia fulani, utahisi hofu kwamba historia itajirudia. Jihadhari na jinsi mambo ya nyuma yanavyoweza kukuathiri. Jiulize “Kwa nini ninahisi hivi? Je! Nina ushahidi gani kwamba mtu huyu mpya atanitendea vibaya?”

Send this to a friend