Mambo 6 ya kuzingatia katika mwezi wa mwisho kabla ya kujifungua

0
26

Kuwa mzazi ni mojawapo ya zawadi kubwa zaidi ulimwenguni. Mwezi wa mwisho katika ujauzito wako ni hatua muhimu kwani ndiyo mwezi uliojawa msisimko na wasiwasi kwa kutambua kuwa baada ya miezi hiyo yote ya kusubiri, mtoto wako atakuja hivi karibuni.

Ikiwa mwezi wa tarehe yako ya kujifungua umefika, zingatia mambo haya machache ili kujiweka tayari;

1. Zingatia mazoezi ya pumzi
Natumaini umekuwa ukifanya hivi kwa wiki kadhaa tayari, lakini ikiwa hujafanya ni wakati wa kuanza. Zingatia kupumua polepole kwa kina. Vuta pumzi kwa hesabu nne, pumua kupitia pua yako na uitoe nje kupitia mdomo wako.

2. Achilia mwili wako
Kuzoeza mwili wako kuachilia na kupumzika kutasaidia sana wakati wa kuanza mchakato wa kujifungua, kwa sababu kuuweka mwili wako katika hali ya utulivu ni muhimu ili kufanya kazi kwa ufanisi.

Acha mikono yako ining’inie, tikisa miguu yako na ulegeze taya yako.

3. Fanya zoezi
Ikiwa bado unaweza kufanya mazoezi, hakuna sababu ya kuacha, unaweza kufanya mazoezi ya kutembea polepole au haraka. Kumbuka tu kuwa na ufahamu wa kila kitu unavyohisi, ikiwa inakuumiza, basi acha mara moja.

4. Pumzika
Kadiri mwili wako unavyohitaji kuendelea kuushughulisha, pia unahitaji kupumzika ili kujiandaa kwa zoezi la kujifungua. Wakati wa mchana fuata sheria ya 50/50, yaani asilimia 50 ya kujishughulisha na 50 ya kupumzika. Ikiwa hiyo inaonekana kuwa nyingi sana, lenga 60/40.

Mambo 7 ambayo wanaume hawapendi yanapofanywa na wanawake

5. Kuwa na Fikra chanya kuhusu kujifungua
Jitahidi kuwa na mazungumzo mazuri kuhusu masuala ya uzazi. Ikiwa mtu unayezungumza naye hana chochote kizuri cha kusema kuhusu kujifungua au uzoefu wake wa kujifungua, ni wakati wa kuacha kuzungumza. Tumia muda wako kusoma kuhusu hadithi chanya za uzazi na ujipe moyo kwa kile kitakachokuja.

6. Fanya ‘massage’
Tembelea mtaalamu wa massage aliyesajiliwa ambaye ana utaalam wa kuwafanyia wanawake wajawazito. Massage hulegeza misuli yako, hukusaidia wewe na mwili wako kupumzika na kuongeza mtiririko wa damu. Zaidi ya hayo, itasaidia kupunguza uchungu wowote unaopata. Panga massage moja mara moja kwa wiki kutoka angalau wiki 37 hadi kujifungua.