Mambo 6 ya kuzingatia unapofanya mazoezi barabarani

0
53

Kufanya mazoezi ni njia nzuri ya kuboresha afya yako na kujenga mwili imara. Hata hivyo, ni muhimu kuzingatia baadhi ya mambo ili kuhakikisha usalama na ufanisi wakati ufanyapo mazoezi barabarani.

Hapa kuna mambo muhimu ya kuzingatia;

1. Tumia eneo la watembea kwa miguu
Barabara nyingi zina eneo kwa ajili ya wanaotembea kwa miguu. Eneo hili hutofautishwa na barabara kuu kwa kuchorwa mstari au hutenganishwa na mtaro wa maji.

Kwa sababu za kiusalama ni bora kutumia njia hiyo ikiwa ipo, kuliko kutumia ile yenye magari. Ni salama zaidi kwa sababu haina mwingiliano na vyombo vya moto, hasa ukiwa unafanya mazoezi peke yako au kikundi cha watu.

2. Kimbia upande wa kulia
Ikiwa mazoezi yako yanakulazimisha kutumia barabara ile ile inayotumiwa na magari, kutokana na kutokuwepo kwa barabara za watembea kwa miguu, kwa mujibu wa Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani, Ramadhani Ng’anzi anasisitiza kutumia upande wa kulia.

‘‘Hii itakusaidia kuyaona magari yanayokuja, itakusaidia kuepuka hatari na kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Wakati huo huo hakikisha ukiwa kulia mwa barabara kimbia pembeni kabisa, epuka eneo la katikati,’’ amesema Kamanda Ng’anzi.

3. Uchaguzi wa mavazi
Kuna nguo ambazo ni rahisi kuonekana ukiwa mbali na nyingine ni vigumu kuonekana. Uchaguzi wa nguo za kuvaa kwa ajili ya mazoezi ni jambo muhimu kwa usalama wa mkimbiaji.

Ikiwa anga ina mawingu, nguo nyeusi sio uchaguzi mzuri. Uchaguzi wa nguo unakuja kwa kuzingatia mandhari au hali ya hewa ya eneo unalokimbia. Vaa nguo ambazo ni rahisi kuonekana na madereva wa magari.

Fanya mambo haya 13 kama uko kwenye miaka ya 20+

4. Bendera mbili
Hizi ni bendera za rangi maalumu nyekundu na kijani, zizonawasaidia wafanya mazoezi kuweza kuruhusu gari ipite au wakati mwingne kuisimamisha gari panapohitajika kufanya hivyo.

5. Usitie vifaa vya muziki masikioni
Kusikiliza muziki na kufanya mazoezi ni utamaduni wa kisasa. Kwa baadhi ya watu muziki huwasaidia kuongeza morali wakati wa mazoezi. Lakini ni hatari ikiwa unasikiliza muziki eneo lisilo sahihi.

Uwapo barabarani ni muhimu kutoweka vifaa vya kusikiliza muziki masikioni, hilo litahatarisha uwezo wako wa kusikia honi za magari. Unaweza kusikiliza muziki ikiwa eneo unalofanya mazoezi sio barabarani.

6. Shiriki Semina
‘Elimu huondoa ujinga,’ Jeshi la Polisi nchini Tanzania huandaa semina kwa wafanya mazoezi barabarani. Hizi ni semina muhimu kuhudhuria kwa wale wanaoshiriki mazoezi ya aina hiyo. Semina hizo hutoa mafunzo ya namna ya kutumia barabara na namna ya kushughulika na madereva.

Kamanda Ng’anzi anashauri kutumia viwanja vya kufanyia mazoezi ikiwa hakuna ulazima wa kuingia bararani. Viwanja ni salama zaidi kuliko barabara.

Chanzo: BBC Swahili

Send this to a friend