Mambo 7 ambayo wanaume hawapendi yanapofanywa na wanawake

0
82

Kila jinsia ina sifa ambazo jinsia nyingine hazipendi. Kuna sababu nyingi ambazo hupelekea uhusiano kuvunjika, lakini unapofahamu baadhi ya vitu ambavyo jinsia nyingine haipendi inaweza kusaidia kuepusha mikwaruzano na hatari ya kuvunjika kwa mahusiano yako.

Haya ni mambo 7 ambayo wanaume hawapendi kwa wanawake zao;

1. Kuwaambia marafiki zako kila kitu
Sote tunajua kuwa msichana huzungumza juu ya jinsi anavyohisi zaidi kuliko mwanaume. Ni sawa kuomba ushauri unapohisi kuchanganyikiwa, lakini mwanaume anachukia wakati unajadili uhusiano wako na marafiki zako. Wanaume wengi huthamini faragha, kwahivyo jaribu kutoweka wazi masuala kati yenu wawili.

2. Kukumbushia makosa ya zamani
Unaweza kuwa bado una kinyongo baada ya kuumizwa na yeye, lakini vizuri kujifunza kutokana na makosa yaliyopita. Mkishazungumza na kusamehe hupaswi kushikilia jambo lile lile na kulileta kila mnapokwaruzana isipokuwa kama amekuwa akirudia kosa mara kwa mara na inakusumbua.

3. Kumdhibiti
Wanaume huchukia wakati wanahisi kuwa unajaribu kudhibiti maisha yao na kuchukua muda wao wote. Inawachosha unapouliza kila mara alipo, yuko na nani, na anarudi saa ngapi nyumbani. Hata ukiwa mpenzi wake, inabidi ukumbuke kuwa wewe si mama yake; yeye ni mtu huru ambaye anaweza kujiangalia na sio lazima kuwa na wasiwasi.

Njia 5 za kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa

4. Kufanya vitu kama mtoto
Wanaume hufikiri kuwa wanawake ni wazuri wanapofanya mambo ya kitoto kwa njia ya kufurahisha, wanapenda kuhisi kuhitajika na kwamba unawategemea, lakini isipite kiasi. Wanaume huchukia Kufanya vitu kama mtoto, kugombana, kulalamika na kutokubali wakati umekosea.

5. Kuwazungumzia wapenzi wako wa zamani
Ni sawa kuwa na mazungumzo kuhusu ‘exes’ wako lakini hupaswi kuwataja kila mara mnapokuwa pamoja.

6. Kutowapa umakini
Wanaume wakati mwingine wanahitaji kuangaliwa pia, ikiwa kila siku unatoka na marafiki zako, humjali yeye au mahitaji yake na kumfanya ahisi kuwa ahitajiki kwako bila shaka hatosita kufikiri upya juu ya uhusiano huo.

7.Ujumbe mrefu
Ukitaka kuwa na mazungumzo sahihi na yeye zungumza naye ana kwa ana, usimtumie ujumbe mrefu wa kumsema au malalamiko kwa sababu hatausoma.

Send this to a friend