Mambo 7 ambayo wanawake hawawezi kuvumilia kwenye mahusiano

0
63

Wanawake wamekuwa wakisifika kwa uvumilivu katika mahusiano yao. Lakini kwa wanawake walioendelea na wenye uelewa mpana kamwe hawawezi kuvumilia mambo haya yafuatayo;

Visingizio
Wanawake hawa hawapendezwi na visingizio juu ya mambo. Mwanamume yeyote ambaye ni mzuri sana katika visingizio hawezi kudumu kwa wanawake wa namna hii.

Kutoheshimu.
Kinachowafanya wanawake wa namna hii kuvutia ni heshima waliyo nayo kwao wenyewe. Kamwe hawatavumilia kuzungumziwa au kudharauliwa. Ukikosea ukafanya kitu kama hicho hatajifikiria mara mbili kuondoka kutoka kwako.

Njia 4 za kuwatunza wazazi wako unapokuwa mbali

Kudhibitiwa.
Hawa ni wanawake wa kujitegemea, wana maisha yao wenyewe na hivyo hukuchagua kuwa sehemu ya maisha yake. Usimwambie kile anachoweza na asichoweza kufanya, wapi anaweza kwenda na wapi hawezi.

Uongo
Wanawake wenye uelewa mkubwa hutafuta mahusiano ambayo yanawapeleka kwenye ngazi nyingine katika maisha yao wenyewe. Mara nyingi huwa waaminifu, hivyo hutarajia uaminifu pia kutoka kwa wapenzi wao. Wakikushika kwa uwongo wanahoji ikiwa wanaweza kukuamini au hawawezi kukuamini.

Asiye na msaada
Wanawake wenye kujielewa hupenda kujituma. Ikiwa hauko nyuma yake na kumtia motisha anaweza asikuhitaji katika maisha yake. Wanawake hawa wanathamini zaidi watu wanaoweza kuwapeleka katika ngazi inayofuata na kumsaidia kuona mambo ambayo huenda asiweze kuyaona.

Unyanyasaji wa Kihisia na mwili.
Wanawake hasa wa karne hii hawavumilii mtu yeyote anayewatendea vibaya kwa kuwafokea, kuwadharau au vipigo.

Kupuuzwa
Hutarajia wakati wako na umakini wako kwa sababu yuko tayari kukupa vyake, hawezi kuvumilia kuona ukimpuuza.

Send this to a friend