Mambo 7 ya kufanya kumvutia mwanamke mgumu zaidi kumpata

0
101

Wanaume wengi hudhani kuwa wanawake wanavutiwa na sura nzuri au mvuto wa mwili wa mwanaume pekee, lakini kuna vitu vya muhimu ambavyo mwanamke huvutiwa zaidi kutoka kwa mwanaume.

 

Haya ni mambo 7 ya kufanya kumvutia mwanamke mgumu zaidi kumpata;

1. Hakikisha muda wote unanukia vizuri

Wanawake wanapenda wanaume wanaonukia vizuri, hivyo daima kumbuka kupaka manukato mazuri lakini tu usizidishe. Unaweza kumvutia mwanamke ambaye si rahisi kushawishika.

2. Jaribu kuwa mcheshi

Mara nyingi msichana huzimika kwa mwanaume kwa sababu tu anaweza kumfanya atabasamu.

3. Zungumza kwa busara na kwa kuvutia

Kila unapokutana nae jitahidi mazungumzo yako yawe ya kuvutia kwa kujaribu kujifunza kuhusu mambo anayoyapenda na pia mshirikishe kwa kuuliza maoni yake wakati wa mazungumzo. Usiwe mtu wa kuongea sana.

4. Jiongeze

Kumfungulia mlango, kumsogezea kiti chake anapokaa, kumuuliza maoni yake wakati wa kuagiza, kulipa bili, kumfikisha hadi mlangoni kwake na kadhalika ni mambo unayotakiwa kuyazingatia. Kuwa mvumilivu na mtulivu wakati wa mazungumzo yoyote na jiepushe kufanya mambo madogo yanayoweza kumkera.

5. Muoneshe heshima

Ukiwa naye heshimu maoni yake na pia mshirikishe na umpe kipaumbele katika uamuzi wowote mdogo au mkubwa unaochukua.

6. Mpe usikivu wako kwake

Onesha kumjali, lakini usijali kupitiliza anaweza kupata wasiwasi. Muhimu zaidi, kuwa mkweli. Pia, inapendekezwa kila wakati kumpa pongezi ili kumfanya ajisikie maalum.

7. Onesha mapenzi

Fanya mambo yatakayomfanya avutiwe na wewe kama vile kumshika mkono, kumwachia ujumbe mzuri, kum ‘surprise’ kwa maua au manukato katika hafla maalum kama vile siku yake ya kuzaliwa.

Kumbuka, kwa kufanya hivyo una nafasi zaidi ya kushinda moyo wa mwanamke.

Send this to a friend