Mambo 9 kutoka katika ujumbe wa Krismasi na Mwaka Mpya wa Rais Samia

0
44

Wakristo duniani kote leo wanaadhimisha Sikukuu ya Krismasi ambayo huambatana na shamrasharma mbalimbali huku baadhi ya watu wakisafiri kutoa eneo moja kwenda jingine kwa ajili ya mapumzi au kuungana na familia zao.

Hiyo pia ndio hali ya Tanzania, na hivyo kupelekea Rais Samia Suluhu Hassan kutuma salamu za heri ya Krismasi pamoja na mwaka mpya kwa Wakristo na Watanzania wote, huku akitumia nafasi hiyo kutoa nasaha zake kuhusu kufuata sheria na kulinda amani ya nchi.

Rais ametuma ujumbe huo kupitia ukurasa wa Twitter na Idara ya Mawasiliano Ikulu kwenda kwa mamilioni ya Watanzania.

Mambo 9 ambayo ameyataja na kuwaasa Watanzania katika ujumbe huo ni:

Kusherehekea kwa;

1. Furaha
2. Amani
3. Utulivu
4. Kiasi

Na kuhusu mwaka mpya wa 2022 amewaasa Watanzania;

5. Kuendelea kubaki wamoja
6. Kufanya kazi kwa biddii
7. Kufanya kazi kwa weledi
8. Kufanya kazi kwa kujituma
9. Na kufanya kazi kwa nidhamu

Baadhi ya wachambuzi wanasema namba 6 hadi 9 ni ishara ya hali ngumu kwa watumishi wa umma wazembe na wala rushwa mara baada ya mwaka mpya. Rais Samia amekuwa madarakani kwa siku 281 tangu kuapishwa Machi 19 mwaka huu.

Ibada ya Krismasi kitaifa mwaka huu imefanyika Kondoa mkoani Dodoma

Send this to a friend