Mambo 9 ya kuepuka kufanya kwenye simu au kompyuta ya ofisi

0
56

Wakati mwingine tunaweza kufanya kazi za ofisini majumbani kupitia kompyuta au simu za ofisini, na baada ya kazi unaweza kushawishika kutumia vifaa hivyo kwa ajili ya kujipa burudani kama kutazama filamu na hata kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii na kadhalika na mwingine hutumia kwa ajili ya mambo binafsi.

Lakini je, una uhakika hakuna anayetazama? Ikiwa una kifaa cha kampuni, kuna uwezekano wa kuwa na programu za ufuatiliaji au za uzalishaji zilizosakinishwa (installed), lakini hata kama huna programu za ufuatiliaji kwenye kifaa chako, huduma za pamoja (shared service) zinaruhusu wafanyakazi wenzako, wakubwa wako au wataalam wa teknolojia ya habari kuona kilichofanyika.

Hapa kuna ushauri kutoka kwa wataalam wa usalama uliotajwa na The New York Times na The HuffPost.

1. Epuka kutumia simu iliyotolewa na kampuni kwa shughuli binafsi kama kupiga simu binafsi, kutuma ujumbe binafsi au barua pepe, au kutumia intaneti kwa mambo yasiyo ya kazi.

2. Epuka kupiga picha na simu ya kampuni hata kama unazifuta, inaweza kuhifadhiwa kiotomatiki na kuweza kufikiwa.

3. Usiweke faili binafsi kwenye kompyuta yako. Ikiwa utapoteza kazi, kompyuta yako ya kazi na hati muhimu zinaweza kutumika dhidi yako itakapotokea mzozo wa kisheria.

4. Epuka kutafuta kitu chochote ambacho pengine ni cha kufedhehesha kupitia Google kwenye simu au kompyuta ya kampuni.

Aina 8 za kazi zinazoongoza kuchochea msongo wa mawazo

5. Usifanye mazungumzo binafsi kwenye programu yoyote kwenye kompyuta ya kazi. Epuka kutumia mitandao ya kijamii.

6. Ikiwa upo ofisini au una watu karibu unapofanya kazi nyumbani, hakikisha daima unaifunga kompyuta yako unapokuwa haupo ili kuzuia watu kufikia taarifa za siri au kuitumia kufanya vitu visivyofaa.

7. Jihadhari katika maeneo ya umma. Mtu anaweza kutazama kioo chako na kupata taarifa. Tracy Maleeff, mchambuzi wa usalama wa habari wa The New York Times, pia alipendekeza kutumia VPN kwenye Wi-Fi ya umma.

8. Mambo yasiyofaa na yenye kuchukiza yanapaswa kuwa mbali na kompyuta yako ya kazi, hata nje ya saa za kazi, hayo yabaki kwenye vifaa vyako binafsi.

9. Usifanye kompyuta ya kampuni kama ni yako binafsi. Usibadilishe mazingira ya usalama, na weka taarifa zinazohusiana na kazi pekee.

Send this to a friend