Mambo anayoweza kufanya mtoto aliyemaliza la saba akisubiri matokeo

0
60

Watoto wa darasa la saba leo wamemaliza mtihani ya kuhitimu elimu ya msingi ulioanza jana Septemba 8, 2021 ambapo zaidi ya watoto milioni 1 wamefanya mtihani nchini kote.

Kwa hatua hiyo ina maanisha kuwa wana zaidi ya miezi mitatu kukaa majumbani wakisubiri kuanza kidato cha kwanza kwa wale watakaopata nafasi hiyo kutokana na matokeo. Lakini umejiuliza kati ya leo hadi atakapoanza kidato cha kwanza mwanao au nduguyo atakuwa anafanya nini?

Wengi wanaomaliza elimu ya mingi ni wenye umri miaka 14 au chini ya hapo, hivyo hawawezi kuajiriwa. Hata hivyo, yapo mambo anayoweza kufanya na yakawa na faida kwake katika maisha ya mbeleni.

Jambo kubwa zaidi ni kutumia kipindi hiki kujifunza ujuzi na stadi mbalimbali za maisha. Ujuzi anazoweza kujifunza zipo nyingi sana, kama vile matumizi ya kompyuta, na hii itamjengea msingi mzuri sana kutokana na matumizi teknolojia kuzidi kukua, hivyo katika elimu ya sekondari anaweza kutumia ujuzi aliopata kujisomea zaidi mitandaoni.

Aidha, anaweza kujifunza ujuzi mwingine kama kupiga vyombo vya muziki, mapishi (bila kujali jinsia), usanifu picha (graphic design), kupiga picha, lugha ya Kiingereza na nyinginezo na au mambo mengine ya kufanana na hayo.

Mbali na hilo, anaweza kuanza kujifunza masomo ya kidato cha kwanza, ili kumpa urahisi kwa kuwa hatua moja mbele pindi atakapoanza. Japo chaguo hili si bora sana, kwani ni vizuri ukampa muda wa kupumzisha kichwa kwa kufanya kitu tofauti na ambacho amekuwa akifanya kwa miaka saba.

Send this to a friend