Mambo makubwa atakayoyazungumza Rais Samia akilihutubia Taifa leo usiku

0
33

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Desemba 31, 2021 atalihutubia Taifa na kutoa Salamu za Mwaka Mpya 2022.

Katika hotuba yake hiyo, anatarajia kutoa tathmini ya mwaka 2021 katika masuala mbalimbali yakiwemo masuala ya kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia.

Pamoja na mambo mengine, Rais Samia pia atatoa mwelekeo wa Serikali katika mwaka ujao wa 2022.

Hotuba hiyo inatarajiwa kurushwa mbashara saa 3:00 usiku kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Send this to a friend