Mambo matatu ya kufanya unapozimikiwa na gari njiani

0
75

Wamiliki na madereva wengi hukabiliana na changamoto za kuharibikiwa na magari wakiwa barabarani. Matatizo kama pancha hupelekea watu kupoteza fedha kwa ajili ya matengenezo kwa fundi bila kuwa na ujuzi wa jinsi gani ya kukabiliana na tatizo hilo wao wenyewe.

Hizi ni njia za kukabiliana na changamoto ambazo hutokea mara kwa mara kwenye magari yanapokuwa barabarani.

Badilisha betri iliyokwisha.
Gari likikataa kuwaka, kuna uwezekano mkubwa kwamba betri limekufa au limeisha chaji. Kuna sababu nyingi za tatizo hili kutokea kama, kuacha taa kuwaka kwa muda mrefu, nguvu ya betri haiendani na nguvu ya gari, betri imeingia maji n.k.

Pia unaweza kuwasha gari kwa muda mfupi kwa kufanya yafuatayo;
Tafuta gari lingine kisha zima magari yote mawili. Fungua boneti na uangalie betri ilipo, angalia sehemu za kuunganisha nyaya, halafu toa nyaya zako za kubusti gari.

Ambatisha upande mwekundu (positive) kwenye terminal ya chanya (+) na upande mweusi/bluu (negative) kwenye terminal ya hasi (-). Kisha washa gari la pili kwa dakika tano, washa gari lililokataa kuwaka. Likishawaka liache kwa dakika tano. Toa nyaya ya kubusti kisha endesha gari, endapo litakataa, tafuta duka la betri ili ununue betri mpya.

Mchekeshaji Tiktok alazwa kwa kula buibui

Kubadilisha fyuzi
Ukikuta redio, indiketa au kifaa kingine kinachotumia umeme hakiwaki, kuna uwezekano mkubwa fyuzi imeungua, hivyo fanya yafuatayo;

Fungua boneti utakuta boksi ya fyuzi kwenye bay ya injini au steering wheel. Kama huioni, itafute kwenye muongozo wa gari (owner manual).
Toa mfuniko wa boksi ya fyuzi utaona namba tofauti na rangi kuonyesha nguvu ya kila fyuzi. Tafuta halafu toa fyuzi iliyoungua.

Kubadilisha tairi iliyopata pancha
Ukipata tatizo hili washa taa zako za dharura halafu egesha gari lako kwenye eneo lenye usalama. Toa vifaa vifuatavyo; jeki, bisibisi, lug wrench (ya kufungulia tairi) kisha toa tairi ya akiba kutoka kwenye buti.

Tumia lug wrench kufungua nati za tairi yenye pancha. Weka jeki chini ya gari halafu anza kuipandisha, fungua tairi, weka tairi ya spea halafu hakikisha unaikaza vizuri, kisha shusha jeki.

Tumia lug wrench kukaza nati za tairi zaidi kisha rudisha kila kitu kwenye gari na endelea na safari yako.