Mambo sita yanayochunguzwa na Tume Huru ya Uchunguzi wa Vurugu za Oktoba 29

0
66

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchunguzi wa Vurugu za Oktoba 29, 2025, Jaji Mkuu Mstaafu Mohammed Chande amesema  tume hiyo imepewa jukumu la kuchunguza takriban mambo sita ikiwemo kubaini chanzo halisi cha matukio yaliyofanyika wakati na baada ya uchaguzi.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, amesema jambo lingine ambalo tume hiyo itachunguza ni kujua lengo la walioratibu na kushiriki kufanya vurugu pamoja na kuchunguza madhara yaliyojitokeza wakati na baada ya uchaguzi.

Tatu, ni kuchunguza na kubainisha madhara yaliyojitokeza. La nne, ni kuchunguza mazingira na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na serikali na vyombo vyake, na mtu yeyote au taasisi nyingine katika kubaini na kukabiliana  na yaliyotokea.

Tano, ni kupendekeza maeneo yanayohitaji kuimarishwa zaidi ili kuongeza uajibikaji wa viongozi na raia kwenye kulinda amani ya nchi yetu, utawala bora, haki za binadamu. Sita ni kuchunguza jambo lolote ambalo Tume itaona kuwa ni muhimu na linaendana na majukumu ya Tume,” ameeleza.

Aidha, Chande amesisitiza kuwa mpaka sasa hakuna ushahidi wowote walionao wala kupokea amri ya mtu yeyote. Hata hivyo, ametoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano kwakuwa majibu yote yapo kwao.

Send this to a friend