Mambo usiyotakiwa kufanya unapoendesha gari la automatic transmission

0
28

Kila siku teknolojia inakua kwa kiwango kikubwa na imekuwa na manufaa mengi kwa wanadamu. Ukuaji wa teknolojia umepelekea urahisi katika kufanya mambo magumu kuwa mepesi. Hili limechangia katika kupunguza muda na nguvu iliyokuwa ikitumika hapo awali katika kufanya jambo hilo hilo kwa kutumia nguvu kubwa.

Kwa upande wa magari, teknolojia imetuwezesha watu wengi kupata urahisi katika uendeshaji wake kwani magari ya sasa ‘automatic’ yamerahisishwa sana tofauti na magari ya ‘manual’ ambayo yalikuwa yakiwatatiza watu wengi.

Kuna tofauti kubwa sana ya kiutendaji kati ya magari haya ya ‘automatic’ na yale ya ‘manual’. Magari haya ya ‘automatic’ ni rahisi sana kuyaendesha kwa kuwa sehemu kubwa ya mfumo wa utendaji wake ni wa kisasa kabisa na hujiendesha wenyewe. Ila kuna vitu vya msingi usivyotakiwa kufanya wakati unaendesha magari haya ili kuongeza maisha ya gear box (Transmission Box).

1.Usiegeshe gari lako bila kuweka Parking Brake (hand brake).
Mara nyingi madereva wamekuwa wakipaki magari yao kwa kuweka gear leaver kwenye herufi P, bila ya kuengage Parking Brake (wengi tunifahamu kama hand brake). Kama wewe ni mmoja wao tafadhali acha kufanya hivyo kwa sababu ‘Parking Pawl’, kichuma kinachoizuia gari kuondoka wakati imewekwa kwenye Park ni kidogo sana na hakijatengenezwa kwa kazi hiyo. Hivyo ikitokea mtu akaligonga gari lako kidogo kuna uwezekano mkubwa wa gari lako likaanza kutembea kama ulikuwa hujalizima. Pia kipande cha Parking Pawl kilichovunjika kinaweza kikaleta matatizo makubwa katika gear box yako. Magari ya sasa yamekuwa na parking brake zinazotofautiana. hizi ni baadhi ya aina tofauti za parking brake.

2. Usibadili Gear ya mbele ‘D’ kwenda ya nyuma ‘R’ moja kwa moja au ya nyuma kwenda ya mbele moja kwa moja bila ya kusimamisha gari kwanza. Simamisha gari lako kabisa kabla ya kuamua kubadili gear ya kutoka mbele na kurudi nyuma au vinginevyo. Kufanya hivyo bila kusimamisha gari lako kutapelekea uharibifu mkubwa katika gear box yako.

3. Hakikisha engine inapata joto la kutosha kabla ya kuanza kuendesha gari lako
Kama ulazima gari lako kwa muda mrefu sana ni bora ukaliacha kwa muda baada ya kuliwasha ili engine ipate joto la kutosha na kufanya vimiminika vyote katika gari kutawanyika na kufika katika maeneo husika katika kiwango stahiki. Hii italifanya gari lako lidumu kwa muda mrefu na itakupunguzia garama ya kufanya marekebisho mara kwa mara.

4.Usiweke gia ya neutral ‘N’ unapokuwa katika foleni
Madereva wengi wa magari ya automatic wamekuwa na dhana ya kuweka neutral ‘N’ wanaposimama kwenye foleni au kwenye taa za kuongezea magari, wakidhani kuwa wanaokoa kiwango cha mafuta kitakachotumika. Kwa kawaida magari ya ‘automati’c yametengenezwa kwa namna ambayo huyawezesha kuokoa kiasi kikubwa cha mafuta. Hivyo ukiiacha kwenye gear ‘D’ haitotumia mafuta zaidi.
Gari inapokuwa katika ‘neutral’ mzunguko wa injini hupungua, hivyo taa zinaporuhusu ama foleni kuanza kutembea na dereva akaweka gear ya Drive ‘D’ gari inakuwa imepungukiwa na kiwango cha mafuta kilichokuwa kikiingia katika injini. Ni sawa na kumuamsha mtu usingizini na kumuamuru akimbie mara moja.

5.Usibadili gear wakati mzunguko wa engine ya gari ni mkubwa
Madereva wengi wamekuwa na tabia ya kubadili gear kutoka Drive D na kuweka neutral N wanapokuwa katika mteremko kwa lengo la kuokoa kiwango cha mafuta kitakachotunika. Hii ni hatari sana kwani hukufanya dereva kushindwa kulihimili gari kwa usahihi. Vilevile kubadili gear wakati mzunguko wa engine ya gari lako ni mkali ni kitu kibaya kwa sababu itasababisha kulika kwa ‘clutch plates’ za ndani ya ‘gear box’ yako na kukuletea matatizo hapo baadae.

Endelea kuchukua tahadhari uwapo barabarani ili kuhakikisha usalama wako na watumiaji wengine wa barabara.