Mambo yatakayojadiliwa Makamu wa Rais wa Marekani akitembelea Tanzania
Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris pamoja na mumewe, Douglas Emhoff wanatarajia kutembelea nchi tatu zs Afrika ambazo ni Tanzania, Ghana na Zambia kuanzia Machi 25 hadi Aprili 2 mwaka huu.
Katika ziara hiyo Makamu wa Rais anatarajia kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo na Rais Hakainde Hichilema wa Zambia ili kujadili vipaumbele vya kikanda na kimataifa.
Miongoni mwa watakayojadili ni pamoja na demokrasia, ukuaji wa uchumi shirikishi na endelevu, usalama wa chakula, madhara ya vita ya Urusi naUkraine na masuala mengine.
Safari hiyo itaimarisha ushirikiano wa Marekani kote Afrika na kuendeleza ushirikiano na juhudi za usalama na ustawi wa kiuchumi. Kwa ushirikiano na serikali za Afrika na sekta binafsi, Makamu wa Rais ataendeleza juhudi za kupanua upatikanaji wa uchumi wa kidijitali, kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na ustahimilivu, na kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji, ikijumuisha uvumbuzi, ujasiriamali na uchumi.