Mamilioni kiganjani mwako na Bingo ya Parimatch

0
46

Na, Mwandishi Wetu.

Kampuni ya michezo ya kubahatisha Parimatch imeamua kuwapa fursa mpya wateja wake kwa kucheza Casino kiganjani ambayo imesheheni zaidi ya michezo 200 mikali ndani yake ikiwemo BINGO na KENO ambazo zimeshika kasi kwa kupendwa na watu wengi.

Hayo yamebainishwa na Afisa Habari na Mawasiliano kwa Umma wa Parimatch Bw. Ismael Mohamed wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano mfupi na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kusema kwamba  kupitia tovuti yao ya Parimatch wataweza kufurahia kucheza na kushinda michezo mingi ya Bingo kwa dau dogo la kuanzia shilingi 400.

“Hakuna haja tena ya kuendelea kusubiria hadi wikiendi ndio utengeneze pesa kwa kubeti kwenye soka, sisi kama Parimatch tumeamua kuwaletea Casino yenye michezo zaidi ya 200 tofauti tofauti yenye kukupa msisimko ambao hujawahi kuupata huko nyuma. Kwa mfano unaweza kucheza mchezo wa Don Bingote ambayo inaanzia dau la Shilingi 400 na kila sekunde watu wanavuna mkwanja wa maana yaani huu sio utani watu wanapiga kiukweli”, alisema Mohamed.

Aidha, Mohamed aliendelea kwa kusema kwamba “utofauti wa Casino ya Parimatch unaanzia kwenye ubora wa mfumo wetu ambao unaendeshwa kisasa zaidi na kuwezesha kupata malipo kwa haraka zaidi sekunde chache tu mara tu unaposhinda na hakuna masuala ya kusubiria hadi kukuche asubuhi”.

Aidha Mohamed pia aliwasisitizia wadau wa Parimatch kuendelea kufurahia kucheza Virtual game na michezo mingine mbalimbali kupitia tovuti yao ambayo itaweza kuwaburudisha na kusisimua.

 

Kwa upande mwingine, Mohamed amesema kuwa Parimatch inaendesha shughuli za michezo ya kubashiri mtandaoni na imesajiliwa na bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania kwa takriban miaka 5 sasa. Kimataifa ipo zaidi ya nchi 15 ikiwa na wateja zaidi ya milioni moja duniani kote.

Send this to a friend