Tetemeko: Mamlaka ya Hali ya Hewa yasema hakuna uwezekano wa kutokea Tsunami

0
65

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa kuhusu hali ya bahari kufuatia tetemeko la ardhi chini ya Bahari ya Hindi lililotokea Agosti 12, majira ya saa mbili (2) usiku, na kusema kuwa hakuna uwezekano wa kutokea Tsunami.

TMA imesema hayo baada ya kupokea taarifa zilizothibitishwa na ‘Geological Survey of Tanzania’ (GST) kuhusu tetemeko la Ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha 5.9 katika eneo la kusini mashariki mwa Mkoa wa Pwani katika bahari ya Hindi.

Mamlaka hiyo imesema imefanya uchambuzi wa taarifa za tetemeko hilo katika kituo chake cha Tahadhari ya Tsunami na matokeo ya uchambuzi huo yanaonesha kuwa hakuna tishio la Tsunami kutokana na tetemeko hilo. Tetemeko hilo halikuwa
nguvu kubwa na hakuna maporomoko ya ardhi yaliyojitokeza baharini ambayo yangeweza kuzalisha tsunami.

TMA inawashauri watumiaji wa eneo la bahari ikiwa ni pamoja wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyokaribu na bahari ya Hindi kutokuwa na hofu na kuendelea na shughuli kwa kuzingatia taarifa ya hali ya hewa baharini kama ilivyotolewa awali na mamlaka hiyo.

Send this to a friend