Mamlaka yaeleza hatua iliyofikiwa katika kubadili jina la Ziwa Victoria

0
51

Nchi za Afrika Mashariki zinazotumia Ziwa Victoria zinaendelea na mchakato wa kubadili ziwa la jina hilo ambalo ni la pili kwa ukubwa duniani kwa kuwa na maji safi (fresh water) na la kwanza kwa ukubwa Afrika.

Akizungumzia maendeleo ya mchakato huyo Katibu Mtendaji wa Bonde la Ziwa Victoria, Ali Matano amesema mchakato wa kubadili jina la ziwa hilo umefikia hatua nzuri.

Uganda kubadili majina ya wakoloni kwenye mitaa na sanamu

“Ziwa Victoria halikuwa Ziwa Victoria hadi wakati lilipoitwa Ziwa Victoria na wakoloni,” amesema Matano ambapo ziwa hilo lilipewa jina la Malkia wa Uingereza.

Kwa mujibu wa Matano nchini Tanzania ziwa hilo lilikuwa linaitwa Nyanza, Kenya liliitwa Namulondwe na Uganda lilifahamika kama Nalubaale.

“Kwa bahati mbaya baada ya uhuru, baada ya kuitwa Ziwa Victoria, hakuna kikubwa kilichofanyika kubadili jina hilo hadi sasa,” amesema Matano.

Send this to a friend