Msemaji wa Yanga SC, Haji Manara ameonesha kushangazwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kulishishia shutuma jeshi la polisi kwamba utendaji wake unatia shaka.
Katika ujumbe wake aliouweka kwenye ukurasa wa Makonda, Manara amesema kiongozi huyo msstaafu hana uhalali wa kulalamilia mwenendo wa polisi, kwani aliwatumia akiwa madarakani kufanya vitendo ambavyo Manara amedai havikuwa vya haki.
“Mm mwenyew ushawahi kuniweka ndani bila kosa kwa kutumia Polisi hao hao unaowalaumu leo,,,,watu wangapi uliwasweka lock up kwa kutumia cheo chako?” amehoji Manara.
Katika hali ya kushangazwa ameandika, “Leo ww wa kuwasema Polisi? Acha waseme wengine na tulia dunia iendelee kuzunguka ktk Mhimili wake.”
Katika chapisho lake Makonda ameonesha kuunga mkono kauli ya Chama cha Mapinduzi kuwa baadhi ya maofisa wa jeshi hilo wamekuwa na vitendo ambavyo ni kinyume na maadili ya kazi.
“Naunga mkono hoja ya kamati kuu, ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi, wanaolipaka tope jeshi la polisi kwakuwalinda wafanyabiashara MATAPELI wanaodhulumu mali za watu,” ameandika Makonda.
Ameaema “Naomba tuanze na Dar es salaam na mimi PAUL MAKONDA niko tayari kutoa ushirikianao.”
Makonda ameanika hayo baada ya kuzuka mzozo wa umiliki wa kiwanja kati yake na GSM.