Mandonga afungiwa mwezi mmoja, kufanyiwa uchunguzi Muhimbili

0
59

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) imesema bondia wa ngumi za kulipwa, Karim Mandonga hatoshiriki ngumi mpaka atakapopimwa afya yake baada ya kupigwa TKO katika pambano lake na Moses Golola kutoka Uganda lililofanyika Julai 29, 2023 jijini Mwanza.

Akizungumza na Swahili Times, Katibu wa TPBRC, George Lukindo amesema Mandonga anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi Agosti 15 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na majibu ya uchunguzi ndiyo yatatoa majibu endapo ataruhusiwa kucheza pambano lake litakalofanyika Agosti 27 mwaka huu visiwani Zanzibar.

“Kwa kawaida anafungiwa kwanza, mazoezi anaweza kufanya kwa sababu ni afya siyo yeye tu ila kwa sababu Mandonga ni maarufu Tanzania lakini bondia wote wanafanyiwa hivyo hivyo, anafungiwa ndani ya mwezi mmoja anafanyiwa matibabu, baada ya daktari mwenyewe kujiridhisha anaweza akaeleza kama anaweza kuendelea na pambano kama kawaida au la,” amesema.

Al Hilal kumlipa Neymar mshahara mara sita zaidi anaolipwa PSG

Kwa mujibu wa Lukindo Mandonga amefungiwa mpaka Septemba 13 mwaka huu na mpaka sasa hakuna dalili yoyote mbaya ambayo ameionesha ya kiafya baada ya pambano jijini Mwanza.

Send this to a friend