Mandonga amjibu Kaoneka, sababu za kuwa maarufu

0
57

Bondia Karim Mandonga amemjibu bondia Shabani Kaoneka baada ya malalamiko aliyoyatoa kuhusu umaarufu anaoupata Mandonga licha ya kuwa yeye ndiye mshindi katika pambano lililofanyika Julai 30, mwaka huu.

Bondia huyo ameandika katika mtandao wake wa Instagram na kumjibu kuwa hapaswi kulaumu kuhusu mafanikio anayoyapata baada ya pambano hilo kwa kuwa anayepanga kila kitu ni Mwenyezi Mungu.

Kaoneka alalamika Mandonga kuwa maarufu kuliko yeye

“Dah shabani ndugu yangu me naamini kabisa riziki inatoka kwa mafungu na kwa muda maalumu aliyeupanga Mungu suala la nani afanikiwe nani aishie njiani ni majukumu ya Allah.

Mimi na wewe hatupaswi kumlaumu mtu yoyote yule, katika tasnia hii ya mchezo wa ngumi na watu wa media kiujumla hata mimi sijawahi kuwaza kwamba ipo siku nitasimama kama superstar mkubwa but all in all tujifunze kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Kama ipo, ipo tu,” ameandika Mandonga Mtu Kazi.

Send this to a friend