Mandonga: Ushindi wa Muller Jr haukuwa halali, Rais hakufurahi

0
50

Bondia maarufu nchini, Kareem Mandonga maarufu kama ‘Mtu Kazi’ amesema ushindi wa mpinzani wake Muller Jr haukuwa halali na hata Rais wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi hakuridhishwa.

Pambano hilo la ngumi lililofanyika mjini Zanzibar siku ya Jumapili Agosti 27, liliibua hisia za watu wengi likiwa ni pambano la kwanza baada ya kuzuiwa kwa zaidi ya miaka 60 Zanzibar huku Mandonga akishindwa pambano hilo kwa pointi dhidi ya mpinzani wake.

Akizungumza na Swahili Times, Mandonga amesema kuwa “Rais Mwinyi muda wote alikuwa na furaha lakini matokeo yalipotangazwa tofauti akaonekana kuchukizwa” na kwamba anakwenda kujiimarisha zaidi kuhakikisha kuwa katika pambano lijalao anamtoa mshindani wake kwa TKO.

Ommy Dimpoz afunguka ukaribu wake na Diamond

Mbali na Mandonga wengine waliopanda ulingoni ni Dulla Mbabe ambaye alishinda kwa TKO raundi ya kwanza dhidi ya Mussa Banja na Ibrahim Class alishinda dhidi ya Hamis Muay Thai.