Maonesho ya Mboga na Matunda Qatar kuwajengea uwezo wakulima wa Tanzania

0
11

Serikali ya Tanzania kupitia taasisi zake mbalimbali na sekta binafsi itashiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Mboga na Matunda (Doha International Horticulture Expo 2023) nchini Qatar kwa lengo la kutafuta masoko ya mazao ya kilimo.

Maonesho hayo ambayo yamezinduliwa Oktoba 02 mwaka huu nchini Qatar na kuhudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan, yanatoa fursa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kujifunza na kuwekeza katika kilimo hususan kwenye teknolojia rafiki ya mazingira.

Tanzania ni moja ya nchi za Afrika ambazo zimekuwa zikijitosheleza kwa chakula, na sasa imeweka msukumo mkubwa kwenye uwekezaji wa kilimo hasa eneo la upatikanaji wa mbegu bora, miundombinu ya umwagiliaji, utafiti pamoja na upatikanaji wa mbolea nafuu na viuatilifu.

Tanzania kuuza sukari nje ya nchi miaka miwili ijayo

Serikali imebainisha kuwa juhudi hizi zinalenga kupunguza gharama za uzalishaji kwa mkulima na kuongeza tija na uzalishaji kwa ajili ya kutosheleza mahitaji ya ndani na ziada kuuza nchi nyingine.

Sekta ya mboga na matunda ni miongoni mwa sekta zinazokua kwa kasi kwa mwaka kati ya 7% hadi 11% na kutoa fursa za ajira kwa takriban watu milioni 6.5 hasa kwa vijana na wanawake

Send this to a friend