Maoni: Huenda wahitimu wa sasa hawana maarifa yanayotakiwa katika soko la ajira

0
46

Maoni haya ni uzi/thread uliochapishwa na Bwana Given Edward katika mtandao wa Twitter tarehe 20 Novemba 2019. Uzi huu ni moja ya sehemu ya mijadala na maoni mengi kuhusu mtaala wetu wa elimu na mabadiliko ya kiuchumi na kiteknolojia yanaendelea nchini Tanzania na duniani kote, hivi sasa.

________

Changamoto kubwa ni kwamba “mkataba umebadilika”. Kwa muda mrefu  (hata beyond Tanzania) mkataba ulikuwa kwamba

“ukienda shuleni , ukakaa shuleni, na ukafanya vizuri shuleni, utazawadiwa kwa kazi nzuri na hatimaye utaishi vizuri.”

Kutokana na hilo degree ikawa ni kiashiria kwamba you have played your part so the society should play its. And this arrangement made  sense, especially kwa miaka ya nyuma hasa katika nchi za Afrika kulikuwa na uhaba wa wataalamu.

Mfano kwa Tanzania, wakati tunapata uhuru waliokuwa wanajua kusoma na kuandika ni 17% tu, na nchi nzima ilikuwa na mainjinia 12 na madaktari wawili. Kwa hiyo mkataba made sense. Ilikuwa rahisi kuutimiza. Ndio maana wazee wa zamani wanasema walikuwa wanapewa kazi siku au hata kabla ya graduation.

Fast forward miaka 50 mbele, the rules of the game have changed. Wasomi ni wengi, nafasi hazitoshi, mkataba hautimiliziki. Tatizo sasa (na hiki ni kwa mtazamo wangu ndio the philosophical bottleneck of unemployment), ni kwamba we are acting as if the contract is still the same. The rules have changed. Vijana wanaenda shule, wanamaliza, wanauliza “I have done my part, why aren’t you doing yours?”

Na jamii duniani kote zinaanza kuelewa mkataba mpya taratibu. Na mkataba mpya ni kwamba: ukiweza kutengeneza thamani, na kujitofautisha kufikia hatua ya kuwa wa kipekee, utapewa nafasi ya kuboresha maisha yako.

Na hicho ndicho kitu kikubwa ambacho vijana wengi wanahangaika kukifanya – kutengeneza thamani na kujitofautisha. Ndio maana 21st century skills zinasukumwa (haziko kwenye profession yoyote kama uinjinia au udaktari. Zinamsaidia mtu kwenye profession yoyote kujitofautisha).

Pia ndio maana ujasiriamali unashika hatamu siku hizi. Yote ni kutengeneza thamani.  Lakini tatizo kubwa jingine ni kwamba, wazazi wa watoto hawa wameishi kuona mkataba wa zamani ukitimizwa hivyo wanakuwa wagumu kuwaruhusu vijana kujaribu kutengeneza thamani nje ya shule. Nchi nyingi wameanza kuelewa hili na ndio maana hata sera zao za elimu zimeanza kubadilika na kuakisi hili.

Kwa kuzingatia haya yote, tunakuja kugundua kwamba mfumo wa elimu sio mbovu. Unafanya vyema kazi uliyotengenezwa kuifanya. Changamoto ni kwamba kazi tunayotaka ifanye sasa hivi imebadilika. Tunataka itoe watu wanaoweza kujitofautisha huku imetengenezwa kutengeneza watu wanaoweza kwenda shule, kukaa shuleni na kufaulu shule, regardless of the value they are creating.

@Givenality

Send this to a friend