Mapacha wafariki kwa moto wakiwa wamelala ndani

0
67

Familia moja kutoka kijiji cha Cha Ngoo, Mwingi nchini Kenya imeingia kwenye maombolezo kufuatia kifo cha watoto wao mapacha waliofariki katika ajali ya moto uliozuka nyumbani kwao siku ya Jumatano.

Watoto hao wenye umri wa mwaka mmoja na miezi tisa, walikuwa wamelala ndani wakati mama yao alipokuwa amekwenda kwenye duka lake karibu na nyumbani.

Chifu wa eneo hilo, Barnard Musili amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa majirani walijaribu kuzima moto huo lakini hawakuweza kuwaokoa watoto baada ya moto kuenea haraka ndani ya nyumba hiyo.

Miili ya watoto hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwingi, huku sababu ya moto huo ikiwa bado haijafahamika.

Send this to a friend