Mapromota Kenya watishia kuzuia tamasha la Koffi Olomide

0
70

Mapromota wa muziki nchini Kenya wametishia kukatisha tamasha la msanii mkongwe kutoka DR Congo, Koffi Olomide lililopangwa kufanyika siku ya Jumamosi Desemba 09, 2023 kutokana na madai ya fidia yanayotolewa na mapromota hao yaliyotokana na tamasha lililofanyika mwaka 2016.

Mapromota hao, Jules Nsana na Noah Auma Muga wa Nsana Production wamedai Olomide alikiuka makubaliano ya tamasha la Machi 2016 na wanataka kurejeshewa dola 65,000 [TZS milioni 162.8] ama la tamasha hilo hilo lililopangwa kufanyika katika Ukumbi wa A.S.K Dome, jijini Nairobi Show Grounds halitofanyika.

Mwimbaji huyo wa rumba mwenye umri wa miaka 67 alizuiwa mwaka wa 2016 kutoa burudani nchini Kenya baada ya kushutumiwa kumpiga mmoja wa wanenguaji wake wa kike, na hii itakuwa mara ya kwanza kwa Olomide kurejea kutumbuiza nchini Kenya tangu tukio hilo.

Kupitia kwa mawakili wake, Olomide amewahakikishia mashabiki wake kuwa tamasha hilo litafanyika licha ya vitisho kutoka kwa mapromota hao.

Send this to a friend