Marafiki watano wapiga picha katika pozi sawa kwa miaka 40

0
66


Mwaka 1982


Mwaka 2002


Mwaka 2012


Mwaka 2022

Marafiki watano waliopiga picha kwenye Ziwa la Copco kando ya mpaka wa California-Oregon mwaka wa 1982, wamekuwa wakipiga picha kila baada ya miaka mitano wakiwa kwenye pozi sawa kwa miaka 40.
Walipiga picha ya tisa siku ya Jumatano Juni 15 mwaka huu, licha ya mmoja wao kuugua saratani hivi majuzi.
Kabla ya picha hiyo marafiki hao walihofia kuwa huenda ikawa picha ya marafiki wanne mwaka huu badala ya mwenzao kupata saratani mwaka 2019.
Marafiki hao waliohitimu katika Shule ya Sekondari ya Santa Barbara, hawakuwa pamoja tangu picha yao ya mwisho waliyoipiga mwaka 2017 kutokana na saratani ya Burney.
Burney hana wasiwasi na afya yake isipokuwa anahofia benchi wanalolitumia kupigia picha kwa miaka 40 kusikia limevunjika.
“Inapendeza kurudi hapa na kujua kwamba saratani haikuweza kumaliza kile tunachofanya,” Burney alisema.
Wakati wanne kati yao wana umri wa miaka 59, Rumer-Cleary ana umri wa miaka 58.

Send this to a friend