Marais wa Afrika waliopoteza maisha kwa ajali ya ndege

0
79

Tukio la ajali mbaya ya helikopta iliyomhusisha Rais wa Iran, Ebrahim Raisi na maafisa wengine, limeleta majonzi makubwa kwa taifa hilo. Ajali hii inaongeza orodha ya matukio ya kusikitisha katika historia ya ajali za anga zinazowahusisha marais na viongozi wa dunia.

Matukio kama haya huacha alama kubwa duniani kote, na mara nyingi huleta mabadiliko katika utawala na mwelekeo wa nchi, kama ilivyokuwa kwa Rwanda katika bara la Afrika.

Hawa ni marais wa Afrika waliofariki kwa ajali za ndege;

  1. Rais Samora Machel (Msumbiji):
    Rais wa kwanza wa Msumbiji, Samora Machel aliaga dunia mnamo Oktoba 19, 1986, baada ya ndege yake, Tupolev 134 ya Soviet, kuanguka kwenye mlima ndani ya mipaka ya Afrika Kusini.

    Ripoti ya Tume ya Margo iliyoundwa na serikali ya Afrika Kusini ilihitimisha kuwa ajali hiyo ilisababishwa na hitilafu, ingawa ripoti hiyo ilikataliwa na serikali za Msumbiji na Soviet.

    1. Rais Juvénal Habyarimana (Rwanda):
      Mnamo Aprili 6, 1994, Rais wa Rwanda, Juvénal Habyarimana alipoteza maisha katika ajali ya ndege karibu na mji mkuu wa Kigali.

    Tukio hilo ambalo pia liligharimu maisha ya Rais wa Burundi, Cyprien Ntaryamira na wengine kadhaa, lilitokea wakati ndege hiyo aina ya Dassault Falcon 50, ilipopigwa na makombora ya kutoka ardhini wakati ikijiandaa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali.

    Tukio hilo la kusikitisha lilichochea Mauaji ya Kimbari ya Rwanda na kifo chake kimesalia kuwa gumzo.

    1. Rais Cyprien Ntaryamira (Burundi):
      Rais wa Burundi, Cyprien Ntaryamira, pia alipoteza maisha katika ajali hiyo ya ndege iliyomhusisha pamoja na Rais wa Rwanda, Juvénal Habyarimana. Tukio hilo lilitokea walipokuwa wakirejea kutoka kwenye mkutano mkuu Dar es Salaam.

    Tofauti na Rwanda ambako ufyatulianaji risasi ulisababisha mauaji ya halaiki, hali nchini Burundi iliendelea kuwa ya amani kufuatia taarifa za kifo cha rais wake.

    Send this to a friend