Marekani imefuta Visa ya Spika wa Bunge la Uganda kisa Sheria ya Kupinga Ushoga

0
32

Marekani imefutilia mbali visa ya Spika wa Bunge la Uganda, Anita Among huku mbunge, Asuman Basalirwa akisema yeye ndiye mwathirika wa kwanza kuwekewa vikwazo baada ya taifa hilo la Afrika Mashariki kupitisha sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja.

“Kuanzia Mei 12, 2023, wewe (Among) huna visa halali ya Marekani ingawa unakaribishwa kutuma ombi tena,” amesema Basalirwa alipokuwa akionesha chapisho la barua hiyo kwa wanahabari bungeni.

Mwanaume aomba mahakama ivunje ndoa yake kutokana na uzuri wa mkewe

Kulingana na Basalirwa, spika amehimizwa kupeleka paspoti yake kwa Ubalozi wa Marekani kupitia wizara ya fedha kwa ajili ya marekebisho muhimu ya visa yake.

“Nadhani walikuwa wanatafuta visa yangu ya Marekani lakini hawakuipata. Kwa hivyo, mwathiriwa wa kwanza ni spika,” Mbunge huyo wa Manispaa ya Bugiri aliongeza.

Send this to a friend