Marekani yachangia TZS milioni 251 kusaidia wahanga Hanang

0
41

Marekani imetoa kiasi cha dola 100,000 [TZS milioni 251.2] kama msaada kwa wahanga wa maafa ya maporomoko ya udongo yaliyotokea wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara.

Kulingana na ripoti ya Serikali iliyotolewa leo, maafa hayo yameua takribani watu 80, na kujeruhi watu 117 kuharibu makazi na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali.

Ubalozi wa Marekani umethibitisha hilo leo kwenye mtandao wa X (zamani wa Twitter), ukisema: “Leo, Marekani imeidhinisha utoaji wa dola 100,000 kwa ajili ya maafa kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi katika Mkoa wa Manyara nchini Tanzania.

Matukio haya yamesababisha vifo vya kusikitisha vya zaidi ya Watanzania 70, kuharibu mamia ya ekari za mashamba na maelfu ya watu kuyahama makazi yao.”

Aidha, Rais Samia Suluhu wakati alipotembelea maeneo yaliyoathirika na maafa hapo jana Desemba 07, alitangaza kwamba watu wenye mapenzi mema wamechangisha jumla yaTZS bilioni 2.5 kwa ajili ya kuwafariji waathiriwa, ikiwa ni pamoja na kusaidia katika ujenzi wa makazi yao.

Send this to a friend